Mkaanga chipsi (mpiga drums) wa bendi ya Twanga Pepepa Abuu Semuhando maarufu kama baba Diana usiku wa kuamkia leo akimtokea mzigoni kupiga kazi alipatwa na ajali baada ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha kugogwa kwa nyuma na Benzi na kumfanya apoteze maisha yake.Pigo jingine kwa wanamuzi wa dansi baada ya kumzika Dr Remmy majuzi.Pichani abuu semuhando kushoto akiwa na mmoja wa wanachama wa sisiemu katika kipindi cha kampeni miezi michache iliyopita.Maganga One Blog inatoa pole za dhati kwa familia nzima ya marehemu Abou Semuhando,inatoa pole kwa kundi zima la Twanga pepeta kwa kupata pigo hilo,Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi amini.