Arsenal imelazimishwa kwenda sare na Wigan ya magoli 2-2.
Wigan wakicheza nyumbani ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Arsenal kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ben Watson katika dakika ya 18.
Arsenal walikuja juu ya kulisakama lango la Wigan na kuppata mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 39 na 44, kupitia Andrey Arshavin na Niklas Bendtner.
Wakiwa wanaelekea kupata ushindi wa pili mfululizo baada ya kuizaba Chelsea, Arsenal walijikuta wakienda sare baada la mlinzi wa Arsenal Sebastian Squillaci kujifunga, zikiwa zimesalia dakika tisa mpira kumalizika.
Kwingineko Chelsea ilizinduka na kupata ushindi wake wa kwanza baada ya michezo saba, kwa kuifunga Bolton bao 1-0.
Bao hilo pekee lilifungwa na Flourent Malouda katika dakika ya 61.
Liverpool nayo ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Wolves ambao wako mkiani.
Bao hilo pekee lilifungwa na Stephen Ward katika dakika ya 56.
Liverpool ilishindwa kuonesha cheche zake licha ya nahodha Steven Gerrard kurejea uwanjani.
Wolves wamepata ushindi huo kwenye uwanja wa Anfiled ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 26.
Ushindi wa Chelsea umeipeleka timu hiyo hadi na fasi ya nne, juu ya Tottenham. Arsenal imesalia katika nafasi ya tatu, huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na Manchester United katika nafasi ya kwanza, licha ya kuwa pointi sawa na City.