Kiongozi anayesimamia kamati inayotoa tuzo ya amani ya Nobel Thorjon Jagland, amethibitisha hakuna mtu yeyote atakayekabidhiwa tuzo hiyo la mwaka huu kwa niaba ya mshindi Liu Xiaobo ambaye yuko gerezani.
Bw Xiaobo ni mtetezi wa haki za binadamu nchini China. Jagland aliambia waandishi kuwa tuzo hii itahifadhiwa hadi pale bw Xiaobo aweze kuichukua mwenyewe. Ndio mara ya kwanza tangu 1936 tuzo hiyo kutochukuliwa na mshindi au jamaa wa karibu wa aliyetunukiwa.