Ghasia zimezuka katika mji wa Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya klabu ya mchezo wa soka ya TP Mazembe kushindwa katika fainali ya kuania kombe la dunia kwa klabu mjini, Abu Dhabi, usiku wa kuamkia Leo Jumapili.
TP mazembe ambayo ilikuwa klabu ya kwanza kutoka barani Afrika kuwahi kufuzu kushiriki katika fainali ya mashindano hayo ilishindwa mabao 3-0 na klabu ya Inter Milan ya Italia.