Msanii chipukizi anayekuja juu katika fani ya muziki wa kizazi kipya Barnaba wa kikundi cha THT,amewataka wapenzi wa nyimbo zake kuwa wakae mkao wa kula kwani anakuja kitofauti na Single(nyimbo moja) itakayokwenda kwa jina la Tulizana.Kijana Barnaba anasema ngoma hiyo itakula kali na ya kuvutia wasikilizaji.Pichani Barnaba akiongea kwamba shughuli yote ya kuirekodi imekamilika na hivi karibuni anaidondosha redioni.