Baada ya kupokea na tuzo yake ya mchezaji mwenye mafanikio David Beckham alisema haya..."Nina furaha kupokea tuzo hii kutokana na kile ninachopenda kukifanya na ninapendelea kukifanya zaidi, nimefurahi sana."
Kupokea tuzo hii kutoka kwa Sir Bobby, ambaye alikuwepo wakati nikianza kucheza soka, niheshima kubwa."
Aliendelea kueleza,:Soka ni mchezo wa timu nzima. Bila timu na kuungwa mkono nilikokuwa nikipata kwa miaka yote hiyo, wachezaji kama Ryan Giggs na wengine wakubwa, nisingekuwepo hapa kama si wao kuniunga mkono na uwezo wao mkubwa wa kusakata soka."
"Kuichezea England ni moja ya mambo makubwa katika maisha yangu ya uchezaji soka, na kila mara nimekuwa nikicheza chini ya waalimu bora katika maisha yangu yote ya soka."
"Nawajibika kuwashukuru watu wengi, wazazi wangu, ambao walijitolea sana, ambao mara zote walifanya na wataendelea kufanya, familia yangu na rafiki na bila shaka mke wangu na watoto wangu. Mke wangu Victoria si tu kama amenipatia watoto watatu wazuri, lakini ameniunga mkono kila siku."