Jamani hiyoo sahani ya kushoto ndio ilikuwa yangu,maana ukimaliza ni kuongeza tu,kulikuwa na chakula zaidi ya aina 75 kazi kwako.Nyama,Tonge,mbona uma na vijiko vilikomaa!!


Mimi kushoto na Mfadhili mkuu wa Blog ambaye ndie alikuwa mwenyeji wangu aliyenipa mualiko hukoo mkoa jirani.Hapa tuliingia sehemu moja maarufu sana mkoani hapo,nilibahatika kukutana na watu mashuhuri duniani ila kwa ubize wa misosi sikupata hata flash moja.Kazi yangu ilikuwa ni misosi tu,simnajua kijijini kwangu bamia tu!!
Jamani eeeeh huyu ndiye shemaji yangu jamani...Nilipokelewa vilivyo na shemeji,vitumbua vilee huyu ndiye mpishi,nilikuwa mpaka basii,na kwenye mkahawa huu pia sikumuangusha shemeji kwani aliniambia nijihisi nipo Nzega.
Ulifika muda wa kupozi na kupata flashiizz,nilikuwa Flash jamaniii mpaka macho yakachoka.
Wadau kwa kweli hii sehemu sio mchezo,nilijaribu kuizunguka kadri niwezavyo ili kuona kipi kwetu Nzega hakuna,Ni kiota cha ukweli kwani kila Idara ilikamilika.Wahudumu wanaijua kazi yao ipasavyo,kila dakika wanaizungukia meza.kuna sehemu maalumu za kupumzika ukijiona nahitaji nipumzike.Basi nilikuwa najipumzisha kwa staili ya kula flashizz..
Kiota chenye Idara timilifu sehemu za watoto hazikukosekana,wakati mimi na wenyeji wangu tukibadilisha mawazo huku watoto wetu walikuwa wakijiburudisha kwa kucheza michezo yao sehemu hii.
Hapa nilikuwa nikishushia Ice Cream maana koo lilikuwa kavu,nikaona mmh kwanini nisirudie mishikaki ya kuku?Angalia picha za chini hapo napakua mishikaki ya kuku na chini kabisaa nikaanza kujipasua mwanawane.Kwa kweli siwaambii juu ya hiki kiota!! mambo yalikuwa hatari sana,Nakuahidi bwana mdogo Mrisho ukija huku lazima nikulete hapa maana utakula mpaka utaisahau Rock City.