Mwanadada Kim Clijsters toka mji mdogo wa Bree jimbo la Limburg nchini Belgium ametangazwa kuwa ndiye mwanaspoti bora wa dunia kwa upande wa kike kwa mchezo wa tenisi.Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 27 amefurahia sana matokea hayo.Akiongea kwa upole na heshima kubwa mbele ya vyombo vya habari,alivishukuru sana  vyombo vya habari kwa kumpigia kura na wananchi wote waliompa sapoti katika kinyan'ganyiro cha upigaji wa kura.
"Nawashukuru sana wanamichezo wenzangu na tutegemee kukutana tena hivi karibuni katika mashindano yanayotaraji kufanyika kule Australia(U S Open) alimalizia.