Mchezaji nyota wa Ghana na klabu ya Sunderland ya England Asamoah Gyan amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC 2010
Mshambuliaji huyo wa Black Stars alishinda kwa kupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.
Amepata kura nyingi zaidi ya mchezaji mwenzake wa Ghana Andre 'Dede' Ayew, na pia Yaya Toure na Didier Drogba kutoka Ivory Coast na Samuel Eto'o wa Cameroon.
"Nimefurahi sana, hata siamini," amesema Gyan. "Nawashukuru sana mashabiki wote walionipigia kura." ameongeza.