MSONGO WA MAWAZO/STRESS.
Ndugu zangu na wapenzi wa Maganga One Blog popote duniani mlipo kwanza kabisa naomba nikupongeze brother Maganga One kwa kutuburudisha na kutuelimisha kama Blog yako inavyojieleza hapo juu.Mimi ni mmoja wa wapenzi wa Blog yako na nimekuwa kila siku naipekuwa zaidi ya mara kumi ili kujua nini kimejiri nyumbani na duniani kwa ujumla.Bila kupoteza wakati naomba kama kuna wadau wanaweza kunisaidia juu ya hili swali langu,Hivi Tanzania wanajua nini maana ya neno stress?na kama wanajua wanalichukuliaje?Maana mimi hapa Ulaya ninapoishi na ninapofanyia kazi zangu nafanya kazi na wazungu,Pindi nikitamka kuwa nina stress basi huwa makini sana na mimi na kila wakati wataniuliza naendeleaje,nikiwaambia kuwa hapana nazidiwa na siwezi kufanya kazi,huniruhusu na kunisisitiza kuwa kama nitaendelea kuwa na msongo wa mawazo niendele kwa Specialist wa mambo hayo ili niweze kupatiwa suluhu.Sasa huwa nikipata nafuu na kurudia hali yangu ya kawaida huwa najiuliza na kujipa majibu mwenyewe kuwa hawa wazungu ni watu wenye kujua Ubinaadamu kwelikweli,je ingekuwa kwetu ingekuwaje?Naomba wadau mnisaidie juu ya hili,kwani ni muhimu sana,Stress inaweza kukuua taratibu au ghafla hivyo nisaidieni jamani,Je Watanzania wanajua umuhimu wa neno hili?na wanalichukuliaje pindi mtu akitamka kuwa ana stress?.
 Mdau wa Ulaya - (Mpigaji Kadogoo).

         (haya jamani mdau kaomba kusaidiwa yoyote ajibu kwa email ya magangaone@gmail.com )