Kuna baadhi ya watu hushiba sifa na majivuno wapatapo wadhifa kidogo tu.Pichani waziri mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda`mtoto wa mkulima`akivaa buti tayari kuingia shambani kupanda mahindi,pembeni yake ni mjukuu wake akimsubiri babu yake wakijipandie mahindi yao,duuh hii nimeipenda sana Mh Pinda kweli wewe ni mtoto wa Mkulima.
Cheki kwanza alipokaa na nyuma yake kukoje,yani moja kwa moja huyu si Fisadi kati ya Mafisadi,tunapenda viongozi kama hawa waadilifu na wasio na tamaa ya kujilimbikizia makwao,Mzee wa blog hii nakupongeza sana wewe ni kati ya viongozi wa kuigwa.