Oya Oya Oyaaa!! Oyaaa Oyaa Oyaaaaa!!!

Golikipa bora wa mashindano Juma Kaseja mara alipopekea zawadi yake.

Hongereni sana vijana hii ndio kazi nzuri tunayoitaka,Anaonekana akiyasema maneno haya Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Mh Emmanuel Nchimbi.Pichani akimkabidhi Nahodha watimu ya Taifa na aliyefunga goli la ushindi mfano wa hundi Shadrack Nsajigwa . 

Ubingwa raha sana jamani..hivi ndivyo ilivyokuwa jana uwanjani Taifa jijini Dar es salaam.Mrisho Ngassa japo hakucheza kwa kuwa alionyeshwa kadi mbili za manjano ila kwenye kusheherekea alikuwepo.