Jeshi la Ivory Coast limefunga mipaka ya nchi hiyo na kuzuia vyombo vya habari vya nje huku hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeka kuhusiana na matokeo ya raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama ya Katiba kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi kuwa mgombea wa upinzani Alassane Ouattara ameshinda.
Wafuasi wa Rais Laurent Gbagbo walijaribu kuzuia kutoka kwa matokeo hayo yaliyocheleweshwa, wakidai umefanyika wizi wa kura katika eneo la kaskazini.
Muda mfupi baadaye jeshi hilo lilitangaza "fungunga mara moja kwa matangazo ya vyombo vya habari vya kigeni" nchini humo ikiwemo CNN, France24 na Radio France International FM.
Tangazo la matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumapili, limecheleweshwa sana, na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini humo.