Hata kama wewe ni mwanaume ukiingia kichwakichwa unakula mikono ya maana na unakoma ubishi.Bidada Laila Ali,mtoto wa aliyekuwa bingwa wa dunia katika fani ya ngumi anaelezea jinsi anavyopambana na wanadada wenzie ulingoni.Anasema kuwa anapokuwa ulingoni huwa hatumii mfumo(style) ya baba yake kwa kuremba pambano.Akipanda ulingoni kazi huwa ni moja kuhakikisha anashinda pambano kwa hali zote,anasema huwa anachukulia pambano kama ni vita hivyo hafanyi hajizi kabisaa kuwaangusha wakinadada ulingoni kwa makonde ya uhakika."Najua weakness(udhaifu)wa wanawake na najua wapi nipige hasaa ili mpinzani wangu akae kitako".Nashukuru kuwa kocha wangu ni mzuri na mimi pia namuelewa vizuri kwa hiyo nashukuru kwa hilo na nashukuru kila mara kupata sapoti ya baba yangu.Kila mara kabla sijapanda juu ya ulingo huwa anakuja chumbani kwangu kwa kubadilishia nguo(dressing room/changing room)na kunipa mawili matatu nini cha kufanya kama nyongeza,nami huwa sifanyii hajizi maagizo ya baba.