Timu ya taifa--Kilimanjaro Stars, leo inashuka dimbani kuivaa timu ya taifa ya Ivory Coast fainali ya Kombe la Chalenji, huku kasi yake ya ushambuliaji ikipunguzwa nguvu kufuatia winga Mrisho Ngassa kuwa na kadi mbili za njano ambazo zitamfanya kukosa mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ngassa aliyejuu kwenye kiwango chake cha uchezaji na kutoa mchango mkubwa ulioiwezesha Stars kucheza hatua ya fainali, juzi alikumbana na kadi nyingine ya njano kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Uganda, ikiwa ni ya pili baada ya ile ya kwanza kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Rwanda.