Kwa binaadamu wote lazima tujue kwamba ili tujikomboe katika wimbi la umasikini lazima tujitume sana katika kufanya kazi zetu.

Ikiwa unafanya kazi iwe ya kuchimba mitaro basi uchimbe mitaro kiukweli,ukiwa unauza biashara ndogondogo basi jitume sana kuuza bianshara yako kwa kuamka asubuhi sana na kuhakikisha unaifanya vilivyo ili kukuletea faida.Kama ni mfanyakazi wa serikali jitahidi kufanya kile unachopaswa kukifanya kwa hali zote bila ya uvivu na visingizio visivyo na msingi.

Umasikini unachangiwa sana  na uvivu,na waafrica wengi sana tumekuwa wavivu kwa kila sekta ya uzalishaji.Blog ya Maganga One imekumbushia tu kwa wale wote waliojisahau wakumbuke wajibu wao. Ahsanteni.