Vijana wengi safari zao toka Afrika huishia hapa na kurudishwa nyumbani.Ni uwanja mkubwa sana na wenye abiria wengi kweli,tatizo la hawa jamaa zetu wakikuona mweusi tu inakuwa mtihani kwako,kama hujui kujieleza vyema aaah unageuza na Next fright.kukurudisha kwenu wao wanaona ni kitu cha kawaida tu,wala hawajui kama umetumia gharama kiasi gani yani wao ni kukurudisha tu.Nazungumzia Uholanzi wajameni.Kivumbi kinakuja paleee mnapoambiwa ndege imesitisha safari zake mpaka baada ya masaa manne,wakati wewe umeingia airport saa tisa za usiku.Hii ni pale Schiphol airport,Amsterdam nchini Holland.