Kila siku ya jumatatu wanafunzi wanakwenda kuogelea,Hili basi pichani linawasubiri wanafunzi kwenda kuogelea,huwa linawachukua na kuwarudisha shuleni...Mabasi kama haya kwa uhakika wa fikra zangu labda,labda ipande Taifa stars au kama tuna Ugeni wa timu kubwa kama Brazil  hivii ndio tutakodi na kuwapandisha wao na sio watoto wetu ambao wanahitaji vitu kama hivi tokea wadogo.Tujifunze kuwa tunawazoesha watoto mambo kama haya ili kuwajengea misingi mizuri tokea wakiwa na umri mdogo.Na wenye mabasi tafadhali wekeni viwango vya chini vya kukodisha mabasi yenu ili kila mmoja aweze kumudu gharama hizo.Picha hii ni kwa wenzetu sio Africa wajameni.