Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema, amepigwa na kuumizwa vibaya na kusekwa rumande baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na kupingwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha.
Lema anadaiwa kupigwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji kwa kushirikiana na Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU).
Tukio hilo lilitokea jana mara baada ya uchaguzi huo kushindwa kufanyika juzi baada ya CCM kudaiwa kulazimisha Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho kupitia Mkoa wa Tanga, Mary Chatanda, ambaye pia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, kutaka kupiga kura kumchagua Meya wakati yeye si Mbunge wa Arusha.
Sakata hilo lilipofika jana, CCM wakiwa na diwani wa chama cha TLP, walipiga kura bila kuwepo wawakilishi wa chama cha Chadema, na kumteua Meya kwa tiketi ya CCM, Gaudence Lyimo aliyeshinda kwa kura zote 17 na Naibu Meya Michael Kivuyo wa TLP ambaye alipata kura 17.
Mara baada ya uchaguzi huo kufanyika, Chadema wakiongozwa na wabunge wao watatu, waliingia ukumbini na kukuta Meya mteule na Naibu Meya wako mbele, ndipo waliposimama na kupinga uchaguzi huo kwa kuwa sheria za uchaguzi huo ni lazima ufanyike kwa kufikia wajumbe theluthi mbili ya wapiga kura, ambapo CCM hawakufikia licha ya kuwepo wa TLP.
Wakati Mbunge wa Chadema, Lema akiongea ndipo madiwani wa CCM walipomwita OCD nje ya ukumbi aingie ndani kwa madai Mbunge anawaingilia kwenye kikao chao na hapo OCD alipoingia na kumshika Mbunge huyo huku akimpiga virungu, jambo lililozua tafrani na kuchapana makonde.
Wakati wanachapana makonde, ghafla kiliitwa kikosi cha FFU na kuingia ndani ya chumba hicho na kuanza kumpiga Mbunge huyo kwa marungu na mateke, hadi kupoteza fahamu na kumwingiza kwenye gari lao.
Hali hiyo ilizua tafrani na kusababisha madiwani wa chama cha Chadema kuhamaki na kuanza kusukumana na polisi.
Hata hivyo, akiongea kwa huzuni, kiongozi wa chama cha upinzani kutoka Chadema, Diwani wa kata ya Elerai, John Bayo, alisema kuwa wao kama chama, kesho (Jumatatu) wanakwenda mahakamani kupinga uchaguzi huo kuwa ulikuwa batili na haukufuata sheria.
Alisema kuwa tayari wamemtafuta mwanasheria wa Chadema, Albert