NDEGE IKIELEKEA LONDON KUPITIA DUBAI.
Baada ya dakika takribani 45 za kumbembeleza mmoja wa abiria aliyegoma kuhama first class na kwenda kukaa sehemu yake ya Economy class kwenye ndege,abiria wengine walianza kulalamika kwanini wanacheleweshwa na safari hiyo!! Wahudumu wa ndege hiyo walijitahidi kadri walivyoweza ila abiria yule aligoma katakata!!
Alipoitwa Pilot wa ndege alitumia dakika moja tu kumnon'goneza yule abiria na kufanikiwa kumuondosha abiria yule mpaka kule economy class.
Mahojiano kati ya abiria na pilot na wahudumu juu ya mbinu gani ya pilot yule aliyotumia kumuondosha abiria yule?Yalikuwa kama ifuatavyo:

Abiria -Ebu tueleze mwezetu umewezaje kumuondosha kwa dakika tu,tena kiulainii?

Pilot - Nimemwambia huku first Class ndege haipiti Dubai,abiria wote wanaokwenda Dubai wapo kule economy Class.
Abiria wote na wahudumu waliangua kicheko ambacho hata mimi mpaka sasa hivi nacheka.
SHULE MUHIMU WAUNGWANA.
                           Mdau wa maganga one blog,Sleyum-Ilala,Dar.