Nikiangalia kushoto na kulia naona miti kila hatua kumi,na nikiangalia vizuri ukingoni mwa barabara naona nyasi nzuriii zilizokatwa kwa ustadi na kuvutia kwa kuipendezesha barabara,nikibaki tena kulia na kushoto nyumba zipo mbali na barabara na zina nafasi ya kutosha kupitisha hewa.Je hii hali kwetu kuvunja nyumba na kuendelea kujenga kiholela itakwisha lini?Kama nakosea msinihukumu naomba mnisamehe ila najaribu tu kuikumbusha jamii yangu na kuwakumbushia wahusika wa idara husika.