Hapa napo ni nchini Uingereza treni zinafanya kazi chini kwa chini,uhakika wa umeme upo masaa 24 na hali ya hewa ni nzuri sana hakuna joto.Kwa kweli viongozi wetu mnapokuja majuu jifunzeni cha kufanya nyumbani,sio kupendezesha maisha yenu tu hali ya kuwa wananchi tunaowapa dhamana ya maisha yetu mnatufanyia mambo yasiyoridhisha.Mimi nina imani kwa kuanzia sehemu ndogo tu inatosha kwani kwa nchi nzima haiwezekani.

Ka nchi ketu kila kukicha bado kanapakatwa na wahisani(kachanga) toka enzi hizoo bado ni ka changa hivi aka ka nchi ketu katakua lini jamani?Wenzetu kuokoa msongamano wa magari njiani wanaamua kujenga chini ya ardhi ambako wanaona kuwa ni njia sahihi kwa matumizi.Tukisema na sisi tuchimbe pale Jangwani mpaka kibaha au hata mbezi inatosha kabisaa kuhepusha msongamano wa magari jamani.Mabasi makubwa yawe yanapita chini na kuibukia mbezi maana siwezi kusema treni ziwe zinapita chini kwani hilo wazo la kununua treni za chini nafikiri mpaka kitukuu cha mjukuu wangu kizaliwe ndipo wazo hilo litafikiriwa.

Hapa ni chini ya ardhi watu wanasubiri usafiri wa kwenda makazini na wengine kurudi majumbani.Ukiangalia jinsi panavyopendeza mpaka mtu unaona raha sana,baadhi ya wananchi hawaoni hii kitu kwani ni vigumu kidogo,sasa kwa viongozi wetu mnaopata nafasi ya kujionea mambo ya wenzetu kwanini nasisi tusiwe angalau na kimoja kati ya kumi walivyonavyo wenzetu?Kwanini misaada tunayoomba tusiwaombe watujengee mambo kama haya?Mbona uwanja mpya wa taifa umejengwa kwa misaada na imewezekana?Naomba nisieleweke vibaya maana najua nchini kwangu,ukisema hivi basi inakuwa balaa,watu tunaogopa kila kitu hii haipendezei jamani maisha ya kutishanatishana haipendezi,ninachosema hapa ni katika hali ya kuitetea maslahi ya nchi yangu.Ahsanteni.