Raia 43 wa Paksitan wametelekezwa mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika daraja la Umoja ililipo Kijiji cha Mtambaswala Wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa.
Inadaiwa kuwa raia hao walitekelezwa katika daraja hilo baada ya kufukuzwa Msumbiji mwanzoni mwa mwezi huu kwa tuhuma za kuingia na kuishi nchini humo bila ya kuwa na vibali.
Inadaiwa kuwa raia hao walisindikizwa na askari wa nchi hiyo hadi mpakani hapo na kuwaacha wakiingia Tanzania Desemba, 3, mwaka huu.habari zaidi gonga chini...
Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mtwara, Nestory Mpota amethibitisha raia hao kutelekezwa mpakani hapo na kwamba ofisi yake iliwashikilia na kuwahoji kati ya Desemba 4 hadi 5, mwaka huu.
" Ni kweli tuliwashikilia raia 43 wa Pakstan tukawahoji na kubaini kuwa waliingia nchini Msumbiji wakipitia mpaka wa Tanzania…walipoingia Tanzania walikuwa na nyaraka zinazowaonesha kuwa ni watalii," alisema na kuongeza kuwa: " Serikali ya Msumbiji baada ya kuwakamata iliwaamuru warudi walikotokea…kwa taratibu za Uhamiaji kule walikoingilia ndipo wanakotokea, hivyo waliwaleta mpakani na kuwatelekeza."
Alifafanua kuwa baada ya mahojiano ya siku mbili na raia hao ofisi yake iliamuru warejeshwe kwao chini ya uangalizi wa askari wa Jeshi la Polisi.
Alisema Desemba, 6 mwaka huu walisafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam. " Hatujawakamata ila tuliwashikilia kwa muda kwa ajili ya mahojiano ….lengo ni kupata taarifa zao muhimu na baada ya zoezi hilo tumewaachia…ni vijana wa umri kati ya miaka 20 hadi 40 walikuwa wanakwenda Afrika ya Kusini kutafuta maisha."