Wakazi wa Temeke jijini Dar es Salaam waliobahatika kushuhudia ‘shoo’ kali ya washiriki wanaochuana katika shindano la Bongo Star Search ‘BSS 2010’ walipata uhondo wa aina yake kwa baada ya kuona vipaji vilivyosheheni vya kuimba nyimbo za wanamuziki mbalimbali na pia kucheza.
Onyesho hilo la kusisimua lilifanyika kwenye viwanja vya Sigara, eneo la Chang’ombe na kuhudhuriwa na umati wa watu.habari zaidi na picha.....gonga chini
Wakazi wa Temeke jijini Dar es Salaam waliobahatika kushuhudia ‘shoo’ kali ya washiriki wanaochuana katika shindano la Bongo Star Search ‘BSS 2010’ walipata uhondo wa aina yake kwa baada ya kuona vipaji vilivyosheheni vya kuimba nyimbo za wanamuziki mbalimbali na pia kucheza.
Onyesho hilo la kusisimua lilifanyika kwenye viwanja vya Sigara, eneo la Chang’ombe na kuhudhuriwa na umati wa watu.
Alisema kwamba kwenda kwake mara kwa mara katika shuguli zinazoambatana na ngoma za rusha roho kutapungua sana baada ya kupata mafunzo yaliyomuongezea ufikiri ndani ya BSS, na hilo anahisi kwamba linaweza kutafsiriwa na baadhi ya mashoga zake kuwa ni matokeo ya maringo na majivuno wakati ukweli ni kwamba yeye si mtu wa tabia hizo.
Chiby alisema kwamba BSS imemuangazia mwanga flani kuhusu stadi za maisha na anaogopa kwamba umaarufu alioupata sasa unaweza kumsumbua machoni mwa baadhi ya watu.
CHRISTABELLA + BELLA
Mshiriki Christabella Nzowa ana matumaini makubwa kwamba mwenzake Bella atajirekebesha tabia kwavile anaamini kuwa kinachomsumbua ni umri wake kuwa mdogo kuliko washiriki wengine wote ndani ya mjengo wa Kili BSS.
Alisema kwamba kwa anavyomuona, anaamini kuwa Bella ana kipaji kikubwa katika muziki, lakini anachosumbuliwa sasa ni utambuzi wa namna Mungu alivyomjaalia vipawa vingi ambavyo wengine wengi hawana.