Kama kawaida Serikali inapotoa agizo lake wananchi ni kufuata tu,Haki na ubinaadamu unachukua mkondo kwa wananchi na wakazi wa maeneo yatakayoathirika na ubobomoaji wa nyumba hizo.serikali imetenga bilioni 11 kwa wakazi watakaovunjiwa kama fidia ya nyumba zao.wamiliki 330 wa mashamba yaliyoko katika maeneo ya Zavala, Nyeburu, Kinyamwezi, Kivule na Kigogo Fresh, nayo yatatwaliwa na serikali kwa ajili ya kuwahamishia wenye nyumba zitakazobomolewa.
Pia wenye mashamba hayo nao watalipwa fidia ya mashamba na mali zao ili kuwapisha wakazi hao wa Kigilagila.
Awamu ya pili ya ulipaji wa fidia hiyo, inafuatia ile ya kwanza iliyohusisha bomoabomoa ya nyumba 293 katika eneo la Kipawa, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupisha upanuzi, kuboresha na kuongeza shughuli muhimu, zikiwamo zinazohusu usalama katika uwanja huo.
Tamko hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama na Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), William Shehambo, walipozungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya jana.