Rais Barack Obama ametia saini sheria ambayo kwa mara ya kwanza itaruhusu mashoga jeshini kuwa wazi na hali zao za kijinsia bila ya kuwa na wasiwasi wa kufukuzwa kazi.
Rais Obama amesema mabadiliko hayo yataimarisha jeshi na kwamba ilikuwa ni hatua sahihi ya kuchukua.
Katika sera ya zamani, iliyojulikana kama "Usiulize, Usiseme" iliruhusu mashoga kufanya kazi jeshini, lakini kwa kuweka hali ya jinsia zao siri.
Sera hiyo ilianzishwa miaka kumi na saba iliyopita wakati wa utawala wa rais Bill Clinton, ikichukua nafasi ya kupiga marufuku mashoga jeshini.

DUUH TUNAKOKWENDA SASA NAONA NI MWISHOOO KABISAA!!eeeh MOLA tuepushe na jeshi letu.