Kijana mdogo mwenye kasi na chenga za maudhi Samir Nasri jana aliifurahisha timu yake ya Arsenal kwa kuifungia goli mbili na kuifanya kuongoza ligi kuu nchini humo.Arsenal ikicheza kwa ustadi na kasi kama kawaida yao walipendezesha mpira na kuonekana mpira mzuri sana kwa siku hiyo ya jana kwa kuwashinda wapinzani wao Fulham.kwa matokeo zaidi ya mechi nyingine zilizochezwa jana
Tottenham licha ya kuongoza kwa muda ikiwa ugenini, imetoka sare dhidi ya Birmingham City, kwenye uwanja wa St. Andrews. Sebastian Bassong ndio alifunga bao la Spurs katika dakika ya 19, huku bao la kusawazisha la Birmingham City likifungwa na Craig Gardner dakika ya 81.
Blackburn Rovers imeiachia kisago Wolves kwa mabao 3-0. Davin Dunn, Brett Emerton na Ryan Nelsen wakifunga mabao hayo.
Chelsea imeendelea kujivuta baada ya kutoka sare ya 1-1 na Everton. Didier Drogba alifunga bao la Chelsea kwa njia ya mkwaju wa penati dakika tatu kabla ya mapumziko, huku bao la kusawazisha la Everton likifungwa na Jermaine Beckford katika dakika ya 86.
Nahodha wa Manchester City Carlos Tevez ameongoza kwa mfano, baada ya kuipatika timu yake bao pekee na la ushindi dhidi ya Bolton.
Na katika mchezo mwingine, Wigan imetoka sare ya 1-1 na Wigan. Mabao ya Wigan yamefungwa na Danny Collins wa Stoke aliyejifunga, na la pili Tom Cleverly. Magoli ya Stoke yamefungwa na Robert Huth na Matthew Ethrington.
Mchezo kati ya Blackpool dhidi ya Manchester United umeahirishwa kutokana na hali mbaya ya hewa kuathiri uwanja.