Mafundi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), wakiifanyia matengenezo injini namba 12 inayozalisha umeme wa megawati 8.73 katika mitambo ya kutumia gesi iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Kwa mujibu wa Meneja wa mtambo huo, Ambakisye Mbangula, matengenezo ya mtambo huo utakamilika katikati ya mwezi ujao.