Mabingwa wa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefuzu kwa fainali ya kombe la klabu bingwa duniani baada ya kuwafunga mabingwa wa Amerika ya kusini- Internacional kutoka Brazil 2-0 mjini Abu Dhabi.
kwa habari na picha zaidi....
TP Mazembe inakuwa klabu ya kwanza barani Afrika kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia,na inasubiri kucheza kwenye fainali dhidi ya mshindi kati ya mabingwa wa ulaya Inter Milan ya Italia na mabingwa wa Asia Seongnam IIhwa kutoka Korea Kusini, ambazo zinachuana Jumatano katika nusu fainali ya pili.
Bao la kwanza la TP Mazembe lilifungwa katika dakika ya 53 na mshambuliaji Mulota Kabangu, naye Dioko Kaluyituka akafunga la pili katika dakika ya 85.
Internacional walipata nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza lakini ngome kali ya ulinzi ya TP Mazembe ikayakomesha mashambulizi yote, na pia mlinda mlango Muteba Kidiaba akaokoa mikwaju mingi.
Fainali ni Jumamosi tarehe 18.