Nchi ngapi hazina Amani,Nchi ngapi zina Uhuru na bado wananyukana risasi?Nini maana ya sikukuu ya Uhuru watu wanakaa tu nyumbani bila hata kusherehekea kwa kupongezana kwa kuulinda uhuru wao na kuishi kwa Amani.
Nchi ngapi ambazo zina Uhuru ila kama hazina Uhuru kwa jinsi wanavyotawaliwa kiakili na mazingira yao?Kama kuna wataalamu wa kuanzisha somo la kila mwananchi kujua umuhimu wa Uhuru basi wajitokeze na kuwafundisha watu wasiojua nini maana ya neno hili.Kwa nchi za wenzetu waliondelea au naweza kusema baadhi ya nchi zilizotawala Africa nao walitawaliwa na nchi nyingine siku za uhuru kwao huwa wanakesha wakishangilia sana na kufanya mambo mazuri ya kufurahisha kila mmoja.Naomba kwa sisi na wengine kupitia ujumbe huu tuwe tunafundishana umuhimu wa siku hii.Ahsanteni.