Wafuasi wa Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, anayeng'ang'ania madaraka, ingawa anachuliwa na ulimwengu alishindwa uchaguzi, wamewashutumu wanamabalozi wa mataifa ya Magharibi, kwamba wanapanga njama ya kulifanya jeshi liache kumuunga mkono Bw Gbagbo.
kwa habari zaidi...
Alassane Ouattara anayetambiliwa na Umoja wa Mataifa alishinda uchaguzi, amemteua Waziri Mkuu, lakini serikali ya Bw Ouattara sasa inalindwa na Umoja wa Mataifa hotelini mjini Adidjan.
Mkwamo katika siasa za Ivory Coast, hauoneshi dalili ya kumalizika haraka.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi akiungwa mkono na Umoja wa Mataifa, amesema kiongozi wa upinzani, Alassane Ouattara, alimshinda Bw. Laurent Gbagbo kwa kura asilimia nane zaidi.
Hivi majuzi Muungano wa Afrika ulitangaza kuisimamisha uanachama Ivory Coast hadi Bw Ouattara akubaliwe kuwa rais.
Lakini Laurent Gbagbo ameonesha amejiandaa kuendelea kuingoza nchi na anaugwa mkono na maafisa wakuu wa jeshi na anadhibiti televisheni ya taifa.
Siku ya Alhamisi, Bw Gbagbo alisema yuko tayari kuzungumza, lakini hadi sasa amekataa kwenda kuishi uhamishoni na inavyoelekea anataka serikali ya kugawana madaraka, jambo ambalo upinzani umekataa kabisa.
Uchumi wa Ivory Coast umeathirika vibaya na pengine ndio utamuangusha Bw Gbagbo, iwapo serikali itashindwa kulipa mishahara ya watumishi wake.
Lakini Bw. Gbagbo anajulika kuwa shupavu kisiasa na inavyoelekea itakuwa shida sana kumfanya ang'atuke.