TIMU ya Yanga imeanza vema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuwashushia kipigo cha mabao 6-1 AFC ya Arusha na kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi.

Ushindi huo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana umewawezesha Yanga, kuwashusha mahasimu wao wakubwa Simba wakifikisha pointi 28 ambazo ni moja zaidi ya wapinzani wao ambao watashuka dimbani kesho kuvaana na Azam FC inayoshika nafasi ya nne ikiwa na pointi 20.(Picha kutoka maktaba).