Uwanja wa ndege wa Domodedovo wa Moscow umetikisika baada ya kutokea mlipuko wa bomu ambapo msemaji wa uwanja huo alisema watu 35 wamefariki dunia.
Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa- 20 wakiwa katika hali mbaya sana kutokana na mlipuko huo, ambapo ripoti zinasema shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejitoa mhanga.
Mchunguzi mkuu wa Urusi alisema magaidi ndio wamehusika na shambulio hilo.
Uwanja huo, ambao una shughuli nyingi katika mji mkuu wa Urusi, upo kilomita 40 kusini-mashariki mwa mji huo.