Kundi la wanamgambo la Al shabab nchini Somalia limepiga marufuku kwa mwanaume yoyote kusalimia kwa kushikana kwa mikono na mwanamke yoyote nchini humo.Wanamgambo wa Al-Shabbab wametangaza kuwa ni marufuku mwanaume na mwanamke ambao hawana uhusiano wa kidugu kusalimiana kwa kushikana mikono, kuongea pamoja au kutembea barabarani pamoja.

Watu watakaokiuka sheria hiyo mpya watacharazwa bakora mbele ya hadhara au kutupwa jela au hata kuhukumiwa adhabu ya kifo.

"Hii sheria sio nzuri, najihisi kama niko chini ya ulinzi, nimeanza kuzipuuza salamu za wanawake ninaowajua kwa kuhofia adhabu ninayoweza kupewa", alisema Hussein Ali, mkazi wa mji wa Jowhar uliopo kusini mwa Somalia.