MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Mr Blue amemshirikisha aliyekuwa mshiriki wa shindano la Bongo Star Search 2010 (BSS), Bella Kombo katika wimbo uitwao Sexy ambao unatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Blue aliliambia gazeti hili kuwa alikuwa akimfuatilia Bella kwa muda mrefu wakati akishiriki katika shindano hilo la BSS na kuongeza kuwa msichana huyo ana kipaji cha pekee.

Wimbo huo umerekodiwa katika studio ya Combination Sound na prodyuza John Water ambapo alisema kuwa wimbo huo ni wa mapenzi na unatarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali.