Siku za nyuma waziri mkuu alikemea sana juu ya maadili ya muziki na mavazi ya wanamuziki wetu nchini,lakini hali hii imeonekana kama imezibiwa masikio na wanamuziki hao kwa staili zao za mavazi na uchezaji wa show zao wanapokuwa stejini.Pichani waziri mkuu Mizengo Pinda siku za nyuma alipokuwa akizungumzia juu ya kuchukizwa kwake na  wasichana wanaoharibu maadili ya mtanzania katika sanaa kwa ujumla.
 Je kweli tunakokwenda ni kuzuri?tunawafundisha nini watoto wetu majumbani?Hivi ni kweli wananwake wananyanyaswa au huwa wanapenda kujidhalilisha wenyewe?Hili ni kundi la band maarufu jijini Dar es Salaam.
Wanadada wakionyesha ufundi wa kunengua kwa staili wanayoiita kisingino,hapo wakiwa wamekunja shingo zao na kunengua kwa staili ya ajabu kwa jamii yetu.