Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen amesema anatarajia ushindi katika mechi yao ya leo ya kuwania ubingwa wa Kombe la Bonde la Mto Nile dhidi ya Burundi kwa sababu "tunawafahamu vizuri".
Poulsen alisema mjini hapa: "Tulicheza na timu bora Afrika, lakini sasa tunakumbana na watu tunaowafahamu vizuri, sidhani kam
Katika siku ya ufunguzi wa mashindano hayo mapya, Stars ilifungwa 5-1 na mabingwa mara saba wa Afrika, Misri, ambao pia ndio wenyeji wa michuano, katika mechi iliyokuwa ya upande mmoja kwenye Uwanja wa Arab Contractors Jumatano.
Lakini wapinzani wao wa leo kwenye Uwanja wa Jeshi, Burundi nao pia walianza vibaya kampeni zao Jumatano kwa kuchapwa 3-1 na timu iliyobeba yosso wengi ya Uganda.
Stars na Burundi watashuka dimbani leo saa 10:45 jioni kwa saa za huku, sawa na saa 11:45 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, katika mechi muhimu kwa timu zote hizo mbili za Kundi A katika kuwania kuingia nusu fainali.
Kocha Mdenmark Poulsen alisema jana kuwa vijana wake wako katika hali nzuri na tayari wameyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mechi dhidi ya Misri ambayo inaundwa na nyota 10 waliotwaa ubingwa wa Afrika Januari mwaka jana nchini Angola.
Shadrack Nsajigwa, nahodha wa Stars, ambaye pia alikuwa na wakati mgumu katika mechi ya ufunguzi baada ya kugeuzwa-geuzwa na winga wa Mafarao, ambaye alifumua shuti lililopelekea beki wa Stars, Nadir haroub 'Cannavaro' kujifunga wakati akijaribu kuokoa, alisema kuwa wameshaelewa wapi walikosea katika mechi yao ya ufunguzi na hawatafanya makosa tena.
Timu ya Tanzania inawafahamu vizuri Burundi baada ya Kilimanjaro Stars kuifunga 2-0 katika michuano ya Chalenji iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Amas Niyongabo, kikosi hicho amekifanyia mabadiliko madogo sana.
Harambee Stars itacheza dhidi ya DRC katika mechi pekee ya Kundi B leo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Polisi.
DRC, ambayo pamoja na Misri ndizo wadau wa soka mjini hapa wanazipa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, imekuja na wachezaji tisa wa klabu bingwa ya soka Afrika TP Mazembe, ambayo pia ilifika fainali ya klabu bingwa ya dunia hivi karibuni.
Kocha wa DRC, Mutubile Santos alisema jana kuwa wanachukulia michuano hiyo kama maandalizi ya fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwaka huu nchini Sudan.
Aliwataja wachezaji hao kuwa ni kipa hodari Kidiaba Muteba (maarufu kwa stali yake ya kushangilia kwa kudundadunda huku akiwa amekaa chini), Mkulukuta Miala, Mabele Biwaka, Mihayo Kazembe, Kimwaki Joel Kasongo Ngandu, Lofo Bongeli, Kanda Deo na Mvete Luyeye.
“Dhamira yetu ni kuchukua kombe, tumekuja tukiwa kamili, huwa hatubahatishi,” alisema Santos.
Kocha wa Harambee Stars, Zedakaya Otieno, alisema yeye si mtu wa maneno bali vitendo, hivyo walianza kwa kuifunga Sudani na leo watafuzu nusu fainali kwa kuifunga DRC na hawahofii wachezaji wa TP Mazembe. Hakuna timu itakayoondoka hata kama itatolewa mapema kwani zote zimelipiwa kuwepo hadi siku ya fainali Januari 17.
a ni tatizo kwetu. Ingawa katika soka lolote linaweza kutokea, lakini hatutapoteza mechi na Burundi."