Bodi ya mamlaka ya maji na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) imeonyeshwa kuchukizwa na upotevu wa shilingi milioni 340 na imekusudia kutomuongezea muda wa mkataba Mkurugenzi wake Justus Rwetebula baada ya kuelekea kumalizika .Mmoja kati ya wajumbe ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa kwa ujumla Bodi imechukizwa na namna Mkurugenzi huyo alivyoshindwa kutoa taarifa kwa Bodi juu ya wizi huo uliofanywa na mhasibu wa MWAUWASA Moses Ndaki.