Alikuwa Hernandez ndani ya dk 26 kipindi cha kwanza alipoipachikia timu inayoongoza ligi kuu nchini Uingereza Manchester United bao la kuongoza.Mpaka mapumziko Manchester walitoka kifua mbele kwa goli 1 - 0.Kipindi cha pili kilianza vizuri kwa timu zote, ila vijana wa Stoke City walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 5 ya mchezo kwenye kipindi cha pili lililofungwa na kijana machachari Whitehead,Hata hivyo Manchester hawakuwaacha Stoke City watambe kwenye uwanja wao wa Old Trafford baada ya mshambuliaji Nani kuiandikia Man U bao la pili na ushindi katika dk ya 61 na kuifanya Manchester kuendelea kuongoza ligi kwa kishindo.Waungwana hii Man ni hatari wajameni tukubali tu.