VIINGILIO katika mechi kati ya Yanga na Simba dhidi ya Atletico Paranaense ya Brazil ni Sh 200,000 kwa kiwango cha juu na cha chini bi sh 5,000.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mmiliki wa African Lyon ambayo ndio iliyoileta timu hiyo nchini Nabil Salim alisema wanaamini viingilio hivyo kwa Watanzania wanamudu kuingia uwanjani kutazama mechi hiyo.