Mrembo anayeshikilia taji la dunia la 'Miss Progress', Julieth William jana alisaini mkataba na kampuni ya ndege ya Precision Air kwa ajili ya kutembelea mikoa iliyoathirika na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Julieth alisema kuwa anategemea kuanza shughuli za kuhamasisha Watanzania kutokomeza unyanyasaji kwa albino mara baada ya kusaini mkataba huo.
"Wazo hili nilikuwa nalo muda mrefu, nafurahi kupata msaada huu kutoka Precision Air ambao utanisaidia kutembelea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha jamii yetu kutokomeza unyanyasaji wa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi," alisema Julieth.

Alisema kuwa anategemea kuanza ziara yake ya mikoani Januari 15 ambapo ataanza kwa kutembelea mkoa wa Shinyanga kabla ya kuzunguka katika mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa.