Msichana mwenye umri wa miaka 31 raia wa Belgium amen'gwatwa mkono pamoja na bega lake baada ya kupitisha mkono kwenye nondo za banda la chui ambapo alikuwa kaisafisha.Dada huyo alishangazwa na chui huyo ambae wanafahamiana vizuri,kwani kila siku ndio kazi yake kusafisha bandani hapo tokea chui huyo akiwa mdogo.Mmiliki na mwalimu wa chui huyo aliposikia kelele alikimbilia sehemu ya tukio hilo na kumkataza chui huyo kuendelea kumtafuta dada yule,chui alifuata amri za mmiliki yule ya kutoendelea kutafuna msichana yule,baadae yule dada alikimbizwa hospitalini na kushonwa sehemu za majeraha yake.Mmiliki wa chui yule akiongea kwa masikitiko"Nimeshangazwa sana na kitendo cha chui wangu kufanya shambulio lile kwa msichana wangu wakazi"baadae mmiliki yule alimuhamisha chui yule na kumpeleka sehemu tofauti.