Pichani raisi wa China Huo Jinato na raisi wa Marekani bwana Barack Obama wakipeana mikono na tabasamu kwa kila mmoja kuashiria makubaliano ya ushirikiana mzuri baina ya nchi zao mbili.
Raisi Obama amesifu kwamba ushirikiano baina ya nchi zao kuwa umekuwa na maendeleo sana kwa siku zinavyozidi kwenda mbele.Bwana Obama aliendelea kwa kusema kuwa Marekani na China zitakuwa katika hali ya usalama sana endapo zitakuwa kitu kimoja,Obama aliyasema hayo wakati akimkaribisha bwana Huo ndani ya Ikulu ya White house nchini Marekani.