Vivutio vikubwa sana kwa wanawake wengi duniani ni kumuona mwanaume mwenye misuli ya kuvutia,kumuona mwanaume mwenye kifua kikubwa na hata wenye sura nzuri na za kuvutia.Sasa huwa najiuliza mara kwa mara juu ya uchoraji wa rangi maalumu kwenye miili ya baadhi ya watu (Tattoo's)Je alama hizi ni mapambo ya kawaida tu au ni Alama fulani za kikundi au makundi fulani!!!??Bado sijapata jibu sahihi juu ya hizi Alama,Ikiwa mtu unataka kujulikana kwa njia mbadala nahisi hii sio alama sahihi.Kuna mambo mengi sana ya kufanya na kuonekana kama ni mtu maarufu,Pindi ukijaribu kuwauliza baadhi ya hawa watu kwanini wanapenda kuchora hivyo walivyo?jibu utakalolipata toka kwao ni NAPENDA NIWE HIVI..Haya kama kimfaacho mtu chake Hongera zao.