Usain Bolt ametangaza atakimbia mbio za mita 200 katika mashindano ya Bislett, mjini Oslo tarehe 9 mwezi wa Juni.Mbio hizo za Ligi ya Diamond ndio za kwanza kuthibitishwa kwa msimu wa mwaka 2011, baada ya kukabiliwa na matatizo ya mguu alipoumia mwaka 2010.
"Kwa vile huu ni mwaka wa kuwania Ubingwa wa Dunia, kila mashindano ni muhimu kwangu katika kujijenga na kujiweka tayari kutetea mataji yangu, " alisema Bolt.