HAKUNA anayeweza kubisha kuwa mtoto Hanifa Daudi Kibavu maarufu kwa jina la kisanii Jennifer aliweza kuicheza vizuri nafasi yake kama mtoto mlozi au mshirikina ndani ya Filamu ya This Is It chini ya Uongozi wa Muigizaji Steven Kanumba kupitia Kampuni yake ya Kanumba The Great Films.

Hanifa ama Jennifer ameweza kuudhihirishia umma wa Watanzania na wapenzi wa filamu ndani na nje ya Tanzania kuwa yeye ni mkali kwa uigizaji akiwa ameigiza filamu yake ya kwanza This Is It na kuibuka na Tuzo ya Muigizaji Bora kutoka katika Tamasha Fupi la Filamu (Mini-Ziff) lililofanyika Zanzibar Desemba 31, 2010 hadi Januari 2, 2011.