Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linadaiwa kukumbwa na kashfa nyingine, baada ya askari wake mmoja kumpiga risasi ya shingoni dereva wa teksi na kumjeruhi.
Askari huyo ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi hilo huku akiwa na bunduki aina ya SMG, alimpiga dereva huyo risasi sehemu ya shingoni
Dereva huyo, Jamal Abdul (32), amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospital ya Selian jijini hapa.
Taarifa za tukio hilo zimeeleza kuwa askari huyo ambaye polisi bado wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, alifika katika eneo la Shivaz, Kaloleni Jumatatu wiki hii majira ya saa 10:00 alfajiri, ambako dereva taksi huyo huegesha gari lake namba T.976 AGZ aina ya Toyota Mark II saloon, na kumtaka ampeleke katika kituo cha Polisi cha Ngarenaro, baada ya makubaliano ya kulipwa Sh. 3,000.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika karibu na kituo hicho, askari huyo alimwamuru dareva huyo kusimama na alimtaka ampatie Sh. 7,000 ili ampe noti ya Sh. 10,000.