Rais wa Sudan, Omar al Bashir, amesema amekubali matokeo ya awali yanayoonyesha wapiga kura Kusini mwa nchi hiyo, wameamua kwa kauli moja kujitenga na Sudan ya kaskazini katika kura ya maoni iliyopigwa kati ya 9 na 15 mwezi huu.(Pichani Omar Al-Bashir akiwa kati ya moja ya sehemu za mikutano yake).
Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye mji wa Kaskazini wa Al-Damir, jimbo la Mto Nile, Rais Bashir amekiri kuwa raia wa kusini wameamua kwa asilimia 99 kujitenga.
Al Bashir aliwataja wale wanaotarajia kunaweza kutokea maasi kama yale yaliyotokea Tunisia kumpindua kuwa wanaota ndoto.