SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) jana lilitoa ratiba ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo watani wa jadi Yanga na Simba watakutana Machi 5 kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyofanyika Oktoba mwaka jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Simba ambayo ilikuwa mwenyeji wa mechi hiyo ilichapwa bao 1-0 lililofungwa na Jerryson Tegete.