Wapiga kura Kusini mwa Sudan wamejitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni itakayosababisha Sudan Kusini kuwa nchi huru na jipya kabisa kote duniani.
Maelfu ya wapiga kura walipiga foleni katika vituo vya kupiga kura hata kabla ya vituo hivyo kufunguliwa.
Rais wa Sudan ya kusini, Salva Kiir, alikuwa miongoni wa waliotangulia mapema kupiga kura.